August 14, 2014

Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo
kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virus”. ugonjwa wa damu kutoganda.
Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa na Damu mwilini,(Viral Haemorrhagic Fevers) Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa
huu hakijulikani. Katika orodha ya watu 10 waliopata kirusi cha Ebola, basi wastani kati ya watano au tisa hufa.
 
 
 Hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani.Ugonjwa huu pia hauna tiba wala chanjo.Hata dawa za jadi hazijathibitika kutibu ugonjwa huu.
Dalili za Ebola
Pale watu wanapopata Ebola, dalili zake za kwanza ni kuonekana kama magonjwa mengine
Dalili za ugonjwa huu ni:-
Homa kali, inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na dogo, mdomoni, masikioni, machoni n.k.
· Kutapika damu
· Kuharisha damu
· Fizi kuvuja damu
· Kutokwa na damu na kuvujia chini ya ngozi. Kwasababu ya kutokwa na damu sehemu za haja kubwa na ndogo, choo na mkojo pia vitaonekanakuwa na damu.

Kuenea kwa Ebola.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kupita njia mbali mbali.
Njia hizi ni:-
· Kuingia mwilini au kugusana na:-
· Mate
· Damu
· Mkojo
· Machozi
· Kamasi
majimaji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na jasho. kugusa mtu aliyekufa kwa ugojnwa wa Ebola kushika/kugusana na wanyama jamii ya nyani. · Kuchomwa na sindano au vifaa ambavyo havikutakaswa Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya
kujamiiana. kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana
na kumhudumia mgonjwa Ebola.
Athari za ebola
· Unasambaa kwa haraka sana Unasababisha vifo vingi kwa muda mfupi · Jamii huingiwa na hofu na wasi wasi na kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida ni gharama kuwahudumia/kutibu wagonjwa. · Mipaka inaweza kufungwa na watu wakashindwa kusafiri kutoka eneo/nchi moja hadi nyingine.
Tiba ya Ebola
Hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu  wanapata huduma bora kutoka kwa madaktari na wauguzi, wengi wao huishi.
 
 
Kinga ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika.Ni muhimu kwa kila mmoja kuwajibika Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu:-

 Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa
mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola. Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na
mpenzi zaidi ya mmoja.

 Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za
Ebola
uwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu. Wananchi wana tahadharishwa kuepuka
kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa kwa Ebola;badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
ufanya ufatiliaji madhubuti wa ugonjwa huu. Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma
muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola
Wagonjwa wa Ebola hutengenishwa na wagonjwa wengine ili
wasipate kuambukizwa.

Zingatia usafi wa mwili na tabia.

KUMBUKA
Ugonjwa wa Ebola ni hatari sana. Unasambaa haraka na unasababisha Madhara na vifo vingi. Epukana nao.

Related Posts:

  • Tazma jinsi Waziri wa Kikwete alivyotishiwa Risasi    Aliyekuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne iliytoongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete, ndugu Adam Malima leo hii ametishiwa bunduki na jeshi la polisi nchini mpaka kufikia hatua ya askari kufyatua risasi ha… Read More
  • Mwandishi wa habari auwawa    Muandishi wa habari aliyekuwa akiandika na kuripoti habari za uchunguzi zinazohusu madawa ya kulevya na ulanguzi nchini Mexico ameuwawa. Javier Valdez, aliyewahi kushinda tuzo mbali mbali za uandishi wa hab… Read More
  • Brand New Video: Yatima wa mapenzi - Jastine   Tumekuwekea Video mpya ya msanii chipukizi kabisa anaitwa Jastine, wimbo unaitwa Yatima wa mapenzi    … Read More
  • Brand New Video: Korede Bello - Butterfly   Mkali wa muziki na kipenzi cha warembo kutoka nchini Nigeria, Koredebello amekuja na kibao kingine kiitwacho Butterfly. Koredebello ni mmoja ya wanazmuiki wanaoaminika sana nchini Nigeria na Afrika kwa sasa ikiwe… Read More
  • Jeef B - Kwetu Cover by Rayvanny   Mwanamuziki chipukizi Jeef B, Amefanya Cover ya wimbo wa kweti wa mwanamuziki tpoka WCB Rayvanny  Boy, ila kwa upande wa Jeef B, ameimbia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Iohn Pombe Magufuli … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE