Stanslaus Mabula.
Jimbo la Nyamagana Mwanza ambalo lilikuwa chini ya mbuge Ezekiel Wenje lipo kwenye headlines sasa hivi ambapo matokeo ya uchaguzi mkuu 2015 Stanslaus Mabula aliyekua Meya wa Mwanza, yamemtangaza mshindi.
Baada ya ushindi huo wa Mabula, Ezekiel Wenje ameyazungumza haya mbele ya Waandishi wa habari
>>> ‘Tulikubaliana
kwamba wale vijana waliokua wanafanya kazi ya kuingiza yale matokeo
waende kuchukua wino waje waweke palepale ofisini waje waprint ili kila
mgombea apate matokeo yote walivyoingiza kwa kila kituo na kila kata
alafu tujumlishe jumla tupate mshindi‘
‘Wale vijana walivyoondoka kwenda
kuleta wino, aliyesimamia uchaguzi akasimama akasema hakuna haja ya
kusubiri… wakaja na matokeo ambayo sio hata kwenye ile list rasmi, kuna
vitu vingine waliandika pembeni ambavyo tayari walishasave ndio
wakafungua… pia wiki mbili kabla ya uchaguzi walimuhamisha mkurugenzi wa
jiji la Mwanza Hassan Ida na kumpeleka TAMISEMI, kanuni inasema mtu
yeyote anaesimamia uchaguzi hatoamishwa mpaka uchaguzi uishe‘ – Wenje
Ezekiel Wenje usiku wa October 26 2015 alipokataa kusaini kukubali matokeo ya jimbo la Nyamagana.
‘Sheria inataka kura
ikishapigwa pale wanapojumlisha matokeo wakishamaliza kujumlisha yale
matokeo yanatakiwa kuwekwa kwenye fomu (Namba 21 kwa kura za Mbunge)
lakini kwa masikitiko makubwa kuna kata nyingi sanasana kata ya Igoma na
Kishiri Mawakala wetu walinyimwa hizo fomu‘ – Ezekiel Wenje.
Kwenye sentensi ya mwisho Ezekiel Wenje ametangaza kwenda Mahakamani kupinga matokeo hayo na kusema >>> ‘tunajiandaa na Mawakili wetu ili waandae kesi, ushahidi tunao‘
0 MAONI YAKO:
Post a Comment