Idadi ya watu waliofariki kufikia
sasa katika janga la kimbunga kilichopiga kisiwa cha Fiji Jumamosi
iliyopita imepanda na kufikia 42.
Maafisa nchini humo wanahofu
kuwa huenda idadi hiyo ikapanda zaidi, kwani data za watu waliofariki
zinatoka maeneo ya ndani zaidi vijijini.
Nyaya ya nguvu za umeme iliyokuwa imekatizwa sasa inaunganishwa huku vyumba vya kuhifadhia maiti vikiwa bado havina umeme.
Kwa
sababu hiyo, serikali sasa imezishauri familia zilizopoteza wapendwa
wao, kuwazika au kuzichoma maiti haraka iwezekanavyo, kwa sababu ya
ukosefu wa vifaa vya kuhifadhi maiti.
bas sawaaaaaa
ReplyDelete