June 08, 2016

13266823_882952098517543_720315630_n
Msanii mpya kutoka lebo ya WCB, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa bongo alimkataza kujiunga na WCB.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa alimtumia ujumbe wa simu na kumuuliza kwanini amekubali kwenda kusimamiwa na Diamond.
“Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujaje kwangu,” aliongeza.
Rich Mavoko amekuwa juu tangu alipojiunga na lebo hiyo ya WCB na kuachia wimbo wake ‘Ibaki Story’ unaozidi kufanya vizuri kwenye TV na Radio.

Related Posts:

  • Bomu laua watu 79    Zaidi ya watu 79 wamefariki katika mashambulizi mawili ya bomu yaliyokumba mji mkuu wa Iraq Baghdad. Watu wengine 130 wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamg… Read More
  • Apple kununua Tidal ya Jay Z   Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z Tidal. Kampuni hiyo imeripotiwa kwamba inaangazia wazo la kuinunua huduma hiyo kutokana na ush… Read More
  • Tetesi: Mahadhi nipo tayari kwenda Mazembe Winga wa Yanga Juma Mahadhi amesema yupo tayari kutimkia TP Mazembe endapo timu hiyo itamuhitaji  lakini amewataka watoto hao wa tajiri Moise Katumbi, wakutane na uongozi wa timu yake ya Yanga. Mahadhi ameiambia Go… Read More
  • Polisi wavamia ofisi kuu za chama cha upinzani Maafisa wa polisi nchini Zambia wameripotiwa kuvamia ofisi kuu za chama cha upinzani katika mji mkuu wa Lusaka. Maafisa hao wanaarifiwa kuharibu stakabadhi za kampeni za uchaguzi zilizokuwa zimeandaliwa na upinzani kwa … Read More
  • Balozi wa S Leone atekwa nyara Nigeria   Naibu balozi wa Sierra leone nchini Nigeria ametekwa nyara. Maafisa wa Sierra Leone's wanasema Nelson Williams alitekwa nyara akiwa katika jimbo la Kaduna. Hata hivyo maafisa wa Nigeria wanasema haijbainika wazi… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE