Msanii wa Hip Hop Bongo, Roma amesema kuwa Baraza la Sanaa
la Taifa, Basata limeshindwa kumpatia majibu ya msingi juu ya sababu ya
kufungiwa kwa nyimbo yake ya ‘Viva Roma Viva’.
Msanii huyo amekiambia kipindi cha ‘Hatua Tatu’ cha Times FM kuwa
Basata wameshindwa kumpa sababu za msingi juu ya kufungia wimbo wake.
“Siwasemei wengine lakini mimi nilijaribu kuwauliza Basata kwanini
wamefungia wimbo wangu lakini sikupewa majibu ya msingi na yenye
kueleweka,” alisema Roma.
Basata waliufungia wimbo wa Roma ‘Viva Roma Viva’ mwezi October mwaka
jana kwa madai kuwa wimbo huo umekiuka maadili kutokana na kuchochea
ugomvi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment