
Baraza
Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar
leo limemfuta uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim
Lipumba.
Taarifa kutoka katika mkutano chama hicho unaeleza kuwa, wajumbe wote waliohudhuria wamepiga kura ya kuridhia kufutwa uanachama kwa Prof. Lipumba.
Hatua
hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu Prof. Lipumba kurejea na kusema
kuwa yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho kufuatia maamuzi
yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment