Mtandao maarufu wa kijamii wa Twitter ulianzisha ‘verified accounts’ kwa lengo la kuwasaidia watu mbalimbali kuzitambua akaunti halisi za watu maarufu na wenye high profile walioko katika mtandao huo.Kwa Mujibu wa mtandao wa Digital spy, ulishawahi kuripoti kuwa Twitter wanahitaji kusaidia watu kuzitambua akaunti halisi za macelebrity au watu wenge high profile katika jamii pamoja na biashara zenye majina makubwa, na kuongeza kuwa hii itakuwa ni kwa kundi dogo la watu mashuhuri.
Ili kuitambua ‘kurasa halisi (verified account) ktika mtandao wa Twitter, itakuwa na alama ndogo ya tiki ya rangi ya blue kama verification ya watu maarufu katika jamii wakiwemo celebrities, viongozi wa serikali, waandishi wa habari maarufu, bila kusahahu makampuni au bidhaa maarufu, hivyo inakuwa rahisi kwa mtu kuweza kufahamu kama Akaunti ambayo ameifollow halisi au fake.
Sasa Good news kutoka kwa mwanetu ni kwamba, Mnyama mkali mwenyewe wakuitwa perfecto, CEO & Founder wa perfect255.com amezidi kupiga hatua nyingine katika mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya akaunti yake kuwa verified leo Disemba 18.Perfect Crispin mwenye followers zaidi ya 23,4K anakuwa mtangazaji wa nne baada ya MillardAyo, Salama Jabir na Masoud Kipanya kuwa na akaunti ya Twitter iliyokuwa verified.
Tiki inayotambulisha verified account iliyoonekana na Twitter inafanana na ile ya verified accounts za Facebook pia Instagram.
“Verified” ni habari njema sana kwa mastaa na watu maarufu wote duniani (hasa Tanzania) ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida kutokana na watu wengine kufungua akaunti za uongo katika huku zikionesha kuwa ni zao na hivyo kuwachanganya watu wanaodhania kuwa ni zao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment