Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Bara, Msafiri Mtemelwa
Wakati zikiwa zimepita siku tatu tangu CHADEMA watangaze kuwa
watashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kinondoni na Siha leo
Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea kushikiria msimamo wao wa
kutoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa kuwa sababu zilizowafanya wasusie
uchaguzi mdogo uliopita, bado hazijafanyiwa kazi.
Mtemelwa amesema bado chama hicho kitaendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanya mageuzi katika mchakato wa uchaguzi.
ACT Wazalendo walilalamikia kuwa kuna matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama tawala CCM.
Majimbo ya Siha na Kindondoni yalikuwa wazi baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM mwishoni mwa mwaka jana.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment