Mbwembwe za Haji Manara zimeanza kumponza. Kamati ya Uendeshaji na
Usimamizi wa Ligi, imempa onyo kali Mkuu huyo wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano Simba kwa kosa la kuingia uwanjani.
Kiongozi huyo alifanya kosa hilo Jumapili iliyopita wakati wa mechi
ya watani wa jadi ambapo Simba aliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Yanga.
Katika barua hiyo iliyotolewa imemtahadharisha kiongozi huyo kwa
kuendelea kufanya matukio mengine kama hayo na endapo ataendelea kamati
hiyo itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi yake. Soma barua hiyo hapa
chini:
0 MAONI YAKO:
Post a Comment