Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alipokua
akiendelea na ziara yake mkoani Morogoro akielekea Kilombero amezungumza
na wananchi wa kijiji cha Mang’ula ambapo alisimama na kuzungumza na
wananchi.
Baada ya kufanya mazungumzo na wananchi aliuliza kama kuna mwalimu au
mwanafunzi aeleze changamoto waliyonayo, hatimae mwanafunzi wa Kidato
cha kwanza wa shule ya Sekondari Mang’ula aliyejitambulisha kwa jina
Mlindoka Msangi alisema kuwa shule hiyo ina changamoto ya vyoo.
Rais Magufuli alitoa na kumkabidhi mwanafunzi huyo Milioni tatu
kwaajili ya ujenzi wa vyoo na kumkabidhi mtoto huyo kwa askari polisi na
huku akimwagiza kuhakikishe fedha hizo zinafika shuleni katika shule
hiyo.
Hata hivyo Rais Magufuli aliwataka nao wachangie fedha za ujenzi wa vyoo hivyo ili changamoto hiyo iweke kuisha.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment