July 15, 2014

Stori: Makongoro Oging’ NA MAYASA MARIWATA
KUNA STAA wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa filamu Bongo mwenye asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la Chidy kwa kuingia mitini na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri filamu zake mbili lakini kazi haikufanyika
.
 
Staa wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect.
MALIPO YAFANYWA, KAZI HAKUNA
Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri (editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni.

JAMAA AINGIA MITINI, AMKWEPA WEMA
Habari zikazidi kudai kwamba, baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ndipo wiki iliyopita mlimbwende huyo akalazimika kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar es Salaam.

 
GHARAMA ZA FILAMU
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, alimsikia Wema akisema filamu zote zimemteketezea shilingi milioni 70,000,000 mbali na hizo alizomlipa huyo mhariri wa filamu ambazo zikiingizwa kwenye gharama nzima inafika shilingi 75,000,000.

KAMA ZINGEINGIA SOKONI
Habari zaidi zinasema kwamba kama filamu hizo zingehaririwa mwaka jana na kuingizwa sokoni, Wema angekunja mkobani kiasi cha shilingi 140,000,000 hivyo kurudisha gharama za kuandaa (75,000,000) na faida juu (65,000,000).

WEMA ASWAKWA, AKATAE AU AKUBALI
Kufuatia maelelezo hayo kutoka chanzo chetu, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimsaka mrembo huyo ili afunguke kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alipopatikana na kuulizwa sakata zima hakuwa tayari kupepesa macho, akakiri.

Alisema awali kijana huyo aliyemdhulumu alikuwa mfanyakazi wake katika kampuni ‘mufilisi’ ya Endless Fame, cha ajabu toka ampatie hiyo kazi ya kumtengenezea pamoja na kumkabidhi fedha amekuwa akimchenga toka mwaka jana.
“Mimi nashindwa hata kumuelewa ana dhumuni gani na hizo kazi zangu maana hapo ana kama shilingi milioni 140 zangu, kwa kuwa kila kazi nilikuwa nalipwa shilingi milioni 70, nilishafanya makubaliano na Kampuni za Proin Promotion  na Steps kuwapa filamu zangu lakini yeye ananizungusha, toka kipindi kile sijaende China, nikimuuliza majibu yake siyaelewi.”
WEMA AMWAGA CHOZI, MTUHUMIWA MBARONI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wema aliendelea kulalamika  mpaka kufikia hatua ya kumwaga chozi:
“Juzi kati Mtitu alitaka nifanye naye kazi lakini akanikumbushia Filamu ya Super Star, kwamba hajaiona sokoni mpaka sasa, ndipo nikamuelezea, akasema hawezi kukubali niipoteze kirahisi, lazima nisimame kidete kuipata ndiyo nikaenda naye mpaka Kituo cha Polisi Mabatini kufungua kesi na Chidy akakamatwa siku hiyo hiyo.” 

APEWA SIKU SABA
Wema aliendelea kusema: “Polisi walimpa siku saba ahahakikishe ananikabidhi kazi zangu pamoja na kompyuta  moja ambayo aliichukua ofisini kwangu bila ridhaa ya mimi mwenyewe na akagoma kuirudisha.”

AFISA WA POLISI
Naye afisa mmoja wa polisi wa kituo hicho ambaye alizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini alithibitisha Wema kufungua kesi Mabatini na ikapewa jalada Namba KJN/RB/5850/14 WIZI WA KUAMINIWA 3/7/2014.

“Ukweli ni kwamba zikipita siku saba bila kijana huyo kuleta fedha na kompyuta ya Wema hapa polisi, tutamsaka na tukimkamata sheria itachukua mkondo wake,” alisema afisa huyo wa polisi.
UPER STAR, OMOTOLA ALIFIKA
Kama itakumbukwa sawasawa Filamu ya Super Star ilizinduliwa Juni 24, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar na nyota wa muvi za Nollywood (Nigeria), Omotola Jalade Ekeinde alishiriki.

Source: GPL

Related Posts:

  • Brand New Audio: Mash J ft G-Nako- Taarifa Mkali wa Hip Hop toka mkoani Morogoro Mash J Mperampera ameachia Audio ya wimbo wake wa Taarifa aliomshirikisha G-Nako. Wimbo huo uliofanywa na Producer Vennt Skillz wa Kwanza Record za Mkoani Morogoro Video yake ilian… Read More
  • Move ya kukumbukwa  Kariobu mpenzi msomaji wa ubalozini.blogspot.com. Leo ikiwa ni siku ya jumapili, tumekuwekea move ya Wrong Turn 3: Left for Dead iliyotoka mwaka 2009. Malizia wikend yako kwa kutazama Move hii yua kukumbukwa &nbs… Read More
  • Tazama show ya Jagwa Musi Band   Ni kundi la muziki asili wa Mchiriku toka nchini Tanzania. Ni miungoni mwa makundi machache sana yanayofanya mziki huo wa Mchiriku. Mziki wa Mchiriku ni mziki uliopata umaarufu sana mwanzoni mwa miaka ya 90 mpaka… Read More
  • RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Tisa Mtunzi: Enea Faidy Ilipoishia Sehemu ya 8 ( Bofya hapa Kama Hukuisoma ) ..Mwalimu John alipelekwa makuburini kwaajili ya mazishi ingawa yeye alijiona yuko hai. Dorice alikuwa njiani baada ya kutoroka shulen,… Read More
  • Video: Chindo Man ft Wakazi,Fid Q & Dully Sykes – Torati ya Mtaa Ki ukweli kabisa, ukizungumzia makundi ya mziki wa Hip Hop hapa Tanzania lazima hutaacha kulitaja hili kundi la Hip Hop toka Jijini Arusha linaloitwa Watengwa. Sasa hii leo mtengwa Chindo Man ametuletea wimbo wake unaitw… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE