December 03, 2014

                 Dar yetu 
 Picha kutoka #DARYETU @Daryetu on Instagram

Kama ulisikia kuhusu mauji ya Wanawake mbalimbalikwenye jiji la Dar es salaam utakua ulitamani kujua wanaohusika manake stori zilikua zinaripotiwa tu na taarifa zinazoambatana nazo ni kwamba uchunguzi unaendelea.
Sasa mpaka sasa unaambiwa ni zaidi ya Wanawake 11 wameuawa Dar es Salaam katika kipindi cha miaka miwili na kutupwa barabarani au mitaroni huku miili yao ikiwa imefanyiwa vitendo vya unyama na udhalilishaji.
Kutokana na mauaji kuendelea, Polisi wamefanikiwa kuwakamata watu wawili akiwemo ABOUBAKAR KASSANGA Mkazi wa Mwenge na EZEKIEL ASENEGALA mkazi wa Tandika Dar es Salaam ambao wamekiri kuhusika na vitendo hivyo ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao ambao pia wamekiri kuwauwa wasichana wawili hivi karibuni waliotajwa kwa majina ya WANZE MAKONGORO na JACKLIN MASSANJA wamesema wamekuwa wakiwalaghai wasichana kimapenzi na badae kuwaua.
Katika hatua nyingine Kamishna KOVA ametoa tahadhari kwa wasichana kuacha tabia ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa ghafla na watu wasiowafahamu ambapo tukio la mauaji ya wasichana hao wawili lilitokea Novemba 19 mwaka huu ambapo baadhi ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya wasichana hao vimekutwa mahala wanapoishi watuhumiwa hao.
Kamishna KOVA amesema upelelezi bado unaendelea ili kuunasa mtandao mzima wa uhalifu huo.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Millardayo.com

Related Posts:

  • Never Forget Moro - Hoodbangerz Kufuatia tukio la ajali ya Moto uliosababishwa na Roli la Mafuta na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 75 mkoani Morogoro, tukio lililotokea 10 August 2019 siku ya Jumamosi katika eneo la Msamvu, wasanii wa Hood Bangerz … Read More
  • Hit Song:Watabamba - Jimmy flavour ft Blacqboi beats Jimmy Flavour ni mmoja ya wasanii toka mkoani Morogoro. amefanya nyimbo kadhaa na zikafanya powa sana ndani ya Morogoro. nyimbo kama Zohari,usingoje nikifa, na kushirikishwa nyimbo kadhaa na msanii Agatha Mbale. Lakini … Read More
  • Klabu Bingwa Afrika,Yanga yasonga mbele   Klabu ya YANGA imefuzu hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Towship Rollers ya Botswana. Bao la Yanga SC limefungwa na Juma Balinya ka… Read More
  • Audio: Simanzi - CN Record Huu hapa ni wimbo mwingine wa Maombolezo kufuatia ajali ya Roli la Mafuta Msamvu Morogoro iliyopoteza uhai wa zaidi ya watu 75 … Read More
  • Kombe la Shirikisho Afrika, Azam kanyaga twende   Klabu ya Azam imefuzu hatua ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi Complex, Dar es Salaam. Mabao ya Az… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE