
Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Samuel Nyalandu amemtembelea
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu jijini Nairobi nchini Kenya
kumjulia hali kufuatia mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana
Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
Lazaro
Nyalandu amesema kuwa kwa niaba ya watu wa Singida na Watanzania wote
ametoa salamu za pole kwa mke wa Tundu Lissu kwa kuwa bado hajapata
nafasi ya kumuona kiongozi huyo na kusema anasubiri kama ataweza kupata
nafasi ya kumuona usiku wa leo kama madaktari wataruhusu.
"Nimefika hospitali ya
Nairobi mapema leo kumjulia hali Mh. Tundu Lissu madaktari wanaendelea
kumfanyia matibabu, na bado hatujaruhusiwa kumuona. Kwa niaba ya wana
Singida na Watanzania wote, nimetoa salaam za pole kwa mke wake, na bado
nasubiri uwezekano wa kuweza kuonana naye usiku wa leo endapo madaktari
wataruhusu" alisema Nyalandu

"Cha muhimu zaidi, sote
tuendelee kumuombea Mungu amtendee wema, na kumponya katika majira haya
ya kujaribiwa kwake. Katika yote ndani ya yote, ikawe heri kwake" alisema Nyalandu
Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana
Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma na baadaye
kusafirishwa kupelekwa jijini Nairobi Kenye kwa matibabu ambapo mpaka
sasa yupo huko akiendelea kupata matibabu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment