November 17, 2017

Serikali imepokea hundi ya Shilingi milioni mia moja kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka leo Mjini Dodoma kama hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali katika Kuboresha Mazingira.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo, Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Serikali kuhamia Dodoma, tumeamua kuwa fedha hizi zitatumika katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani kupitia mpango maalum ambao tulishauandaa kama Serikali na sasa tunashukuru wadau hawa kwa kutuunga mkono,” alifahamisha Makamba.
Akifafanua, Mhe. Makamba amesema serikali imejipanga kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika dhana ya mazingira hapa nchini, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.
Aliongeza kuwa sasa ni wakati muafaka kwa wadau kujitokeza kushiriki kikamilifu katika Kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Bw. Sebastian Maganga amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kuhakikisha kuwa wanachangia katika shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo mazingira.
Mpango wetu umeanza kwa kuchangia shilingi milioni 100 kwa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, mchango wetu unalenga kusaidia uboreshaji na ulinzi wa mazingira ambayo ni muhimu kwa maisha ya Watanzania wote,” alisisitiza Maganga
Akifafanua, Maganga amesema kuwa Kampuni yake imetenga milioni 150 katika kusaidia jamii katika sekta za Afya, Elimu na michezo.
Tatu Mzuka ni mchezo wa Kubahatisha ambao umechangia zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kama kodi hivyo kuchangia katika kukuza uchumi.

Related Posts:

  • Official Video: Sihitaji - Strevol Kutoka mji kasoro Bahari Morogoro, maeneo ya Forest ndani ya studio za Kwanza Record chini ya mtayarishaji Vennt Skillz, Mokomoko Movemennt inamdondosha kwenu na kumtambulisha rasmi zao lingine kabisa chini ya Lebo hiy… Read More
  • CUF yajitoa rasmi, waipa nasaa UKAWA Chama cha wananchi CUF, Kimetangaza rasmi kujitoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini. Akitoa taarifa kwa umma Naibu Mkurugenzi wa Habari , Uenezi na Mahusiano ya Umma wa… Read More
  • Mbunge wa Kilosa atoa msaada wa Kisima na Mabati kwa wananchi wake  Wakazi wa Kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wakiwa makini kumsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo Mbraraka  Ba Waziri wakati alipokua akifanya mkutano na wananchi hao akiskiliza kero na kutoa utatuzi… Read More
  • AC Milan Yafungiwa WAKON G­WE wasokanchini Italia, AC Milan wamefungiwa ku­shiriki michuano ya Ulaya kwa mwaka mmoja kuto­kana na kukiuka kanuni za soka. Timu hiyo ilikuwa iki­jiandaa kushiriki katika mi­chuano ya Europa League msimu u… Read More
  • official video: Sio Kama Wao - Agatha ft Joh Mkristo Kwa mara ingine tena Mwanamuziki toka mkoani Morogoro anaitwa Agatha Mbale, anadondosha ngoma yake mpya inaitwa Siyo kama wao. Agatha ameshusha hii baada ya ngoma zake za Shujaa na Mawenge kufanya poa . Tazama hapa c… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE