April 17, 2012


Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi nchini Bw. Adrian Nyangamale (Kulia) akizungumza na wadau wa Jukwaa la Sanaa wakati akiwasilisha mada iliyohusu Sanaa ya Uchongaji na Mchango wake katika sekta ya Utalii nchini.Kulia ni Afisa Sanaa wa BASATA Bw. Malimi Mashili. 

Afisa wa Sanaa kutoka BASATA Bw. Mashili akisisitiza jambo wakati akihitimisha Jukwaa la Sanaa wiki hii. 

Mkurugenzi wa Kundi la Parapanda Art Theatre Bw. Mgunga Mwamnyenyelwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu maendelea ya tasnia ya Sanaa nchini huku akisikilizwa na sehemu ya wadau wa Sanaa. Alieleza kuwa, Tanzania ni nchi ya kwanza kuwa na sera ya Utamaduni katika ukanda wa Afrika Mashariki 

 Mkongwe wa Sanaa za Maonesho nchini ambaye pia ni mjumbe wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Mzee Nkwama Bhallanga akichangia mada kwa umakini kwenye Jukwaa la Sanaa.

Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakiwa kutoitegemea Serikali kwa kila kitu na badala yake waweke mikakati yao katika kutumia fursa zilizopo ili kujikwamua na changamoto zinazowakabili.
Wito huo umetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Parapanda Arts Theatre Bw. Mgunga Mwamnyenyelwa wakati akichangia mada iliyohusu Sanaa ya Uchongaji na Mchango wake katika sekta ya Utalii nchini kwenye ukumbi wa BASATA uliopo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa, pamoja na changamoto zilizopo, Serikali imejitahidi kuweka miundombinu, sera na taratibu mbalimbali za kuongoza sekta ya Sanaa hivyo wasanii hawana budi kutumia fursa hizo katika kujiletea maendeleo na kumaliza matatizo yanayowakabili.
“Wasanii tuache kulalamika, tujipange katika kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na kushirikisha wasomi mbalimbali. Nchi yetu imeweka mazingira mazuri ya kukuza sekta ya sanaa hivyo tuyatumie” alisisitiza Mgunga.
Aliyataja baadhi ya mazingira hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa vyuo mbalimbali vya Sanaa kama vya Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Butimba na vinginevyo ambavyo vinatosha kuzalisha wataalam wa Sanaa na wasanii wenye weledi.
Aidha, aliongeza kuwa nchi ya Tanzania ni ya kwanza kuwa na sera ya utamaduni ikilinganishwa na nchi zingine za ukanda wa Afrika Mashariki.
“Tumeenda Kenya,Ethiopia na Uganda, nchi ya Tannzania inaongoza kwa kuwa na vyuo vingi vya Sanaa lakini pia ni ya kwanza kuwa na Sera ya Utamaduni” aliongeza Mgunga.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Bw. Adrian Nyangamale alisema kuwa, shirikisho lake limejipanga kukuza sanaa za ufundi ili kuweza kuwakomboa wasanii na hatimaye kufikia kiwango cha kimataifa.
“Shirikisho limejipanga kuwa na jumba kubwa la Sanaa za ufundi, vituo vya mikoa vya sanaa, kukuza soko la ndani na nje ikiwa ni pamoja na kuunda chombo cha kuratibu na kudhibiti uuzaji holela wa kazi za wasanii” aliongea Nyangamale.

Related Posts:

  • Upigaji kura waendelea Nigeriamaeneo mengi yanahesabu kura zilizopigwa Upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu nchini Nigeria unaendelea kwenye vituo kadha kwa siku ya pili kutokana na kuwepo matatizo ya kiufundi kwa vifaa vya kukagua kadi za kura jana jumamosi… Read More
  • ZItto Kabwe awaumbua watu uenyekiti ACT Aliyekuwa mbunge wa kigoma kaskazini Ndugu Zitto Kabwe amesema hatagombea nafasi ya Uenyekiti katika chama alichojiunga nacho hivi karibuni cha ACT. Amesema hayo muda mfupi kupitia redio E FM katika kipindikatika mahojiano k… Read More
  • Hiki ndiyo chanzo cha kifo cha Abdu BongeSaa zinahesabika toka Tanzania na familia ya bongofleva ipokee taarifa za msiba wa Abdul Bonge Mwanzilishi wa kundi maarufu la Bongofleva Tiptop Connection lenye wanachama kama Tunda Man, Madee, Dogo Janja na wengine waliopit… Read More
  • Hii inamuhusu yule akari aliyekutwa na fedha bandia Jeshi la Magereza nchini limemfukuza  kazi askari wake wa Gereza Bariadi, Mkoani Shinyanga (pichani) kwa kosa la kupatikana na fadha za bandia kinyume na Sheria za Nchi. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana Mach… Read More
  • Bank ya NBC yatoa misaada kwa Albino Mkuu Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mussa Jallow (wa tano kulia) akikabidhi msaada wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla amba… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE