May 13, 2014


 
  Diva The Bawse ambaye ametoa wimbo wake mpya ‘Mashallah’ siku chache zilizopita, amesema anajiandaa kuufanyia video pamoja na kuanza tour ya kuutangaza wimbo huo.
“Video tunatarajia kufanya na aliyefanya ‘Asante’ ya Ay,” Diva ameiambia amesema.

Ameongeza kuwa kwasasa ameamua kuingia kwenye muziki kwa miguu yote miwili, ndio sababu anatarajia kuanza kufanya tour mikoani kuutangaza wimbo wake.
“Nahitaji kutumia muda mwingi kuutangaza huu wimbo, ambao uko chini ya management ya Sharobaro Recs, na ningependa kuulizwa maswali yanayohusu muziki zaidi kuliko mambo binafsi, nahitaji kuwa na privacy na ku-focus na biashara yangu, maisha yangu ya radio na muziki.”
Diva ameongeza,
“Pia nina meneja mpya anaitwa Kerry Kerwin ambaye anamsimamia Victoria Kimani akiwa hapa Tanzania, na pia niko tayari kuanza kufanya shows za mikoani. Tutahakikisha huu wimbo unafika katika radio zote za mikoani Tanzania na nje, na habari njema ni kuwa ‘Mashallah’ imeanza kupigwa Nairobi.”

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE