May 04, 2014

Mashambulio NIgeria
Majeshi ya usalama ya Nigeria yamewakamata watu kadha katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja kufuatia mashambulio ya mabomu ya hivi karibuni, zikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini humo.
Wengi wwaliokamatwa wanasemekana kuwa raia wa kigeni, lakini hakuna taarifa zaidi za kina zilizotolewa.
Maafisa wameagiza kufungwa shule na ofisi za serikali wakati wa mkutano huo, ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na marais wa Rwanda, Senegal na Kenya pamoja na waziri mkuu wa China Li Keqiang.
Serikali iko katika shinikizo kubwa la kukabiliana na kusambaa kwa ghasia nchini Nigeria.
Mlipuko wa Alhamisi uliua watu 19, wiki mbili baada ya mlipuko eneo la karibu na hapo kuua watu 75.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na mashambulio hayo, lakini wapiganaji wa Kiislam wa kundi la Boko Haram wanatuhumiwa kuhusika na matukio hayo.
Rais Goodluck Jonathan akitembelea eneo lililoshambuliwa mjini Abuja
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Nigeria amesema waliokamatwa Jumamosi wanahojiwa na wametoa "taarifa muhimu."
Boko Haram pia wanaaminika kuhusika na utekaji wa zaidi ya wanafunzi wa kike 200 kutoka shule yao katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Rais Goodluck Jonathan anatarajiwa kulihutubia taifa Jumapili baada ya kukosolewa kwake namna anavyowashughulikia wapiganaji wa Kiislam.
Jumamosi serikali ya Marekani iliwaonya raia kuhusu kuwepo mpango wa kushambuliwa kwa moja ya hoteli za Sheraton karibu na Lagos, mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria.

Related Posts:

  • Matumla afanya kweli Mohamed Matumla akijitahidi kumbana vyema mpinzani wake Bondia Mohamed Matumla amefanikiwa kutoka kimasomaso baada ya kumchapa kwa points bondia mwenzake kutoka nchini China Wang Xin Hua katika mpambano wa raundi 10 uli… Read More
  • Kuhusu ajali ya ndege iliyopindika, kumbe Rubani alikuwa na matatizo ya kiakiliAjali ya ndege Viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugo… Read More
  • Pitio la Magazeti ya leo hii ijumaa march 27Leo ijumaa 27/3/2015 tunakupatia fursa ya kujua kile kilichoandikwa katika magazeti ya leo japo kwa Vichwa vya Habari. Kama ukitakaka habari zaidi pitia katika meza za magazeti zilizo karibu nawe … Read More
  • Muswada tata kupeleka waandishi jela wapita Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bunge limepitisha muswada mchungu kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari baada ya kupitisha Muswada wa Takwimu wa Mwaka 2013, ambao pamoja na mambo mengine unataka mwandishi at… Read More
  • Mtoto wa miaka 2 avunja rekodi Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini India.  Kulingana na vitabu vya kumbukumbu ya rekodi za taifa, Dolly S… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE