Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kusababisha machafuko katika mji mdogo wa Minova.
Wanajeshi
hao wanatuhumiwa kusababisha machafuko yanayoendelea kwenye mji mdogo
wa Minova ulio mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2012.
Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .
Ripoti
ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu
wanawake na wasichana 135. Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la
mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili
waasi na wale wa serikali.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment