
Msanii chipukizi wa
kijiwe cha Matofali jijini Morogoro ajulikanaye kwa jina la Jibwa Kali
akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe
mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani
humo

Msanii chipukizi
ajulikanaye kwa jina la Hamisi Ramadhani aka Brashi Waya 2akionyesha
umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali
mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo.
Pichani ni mashabiki na vijana wa kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro.

Meneja
Uhusiano wa Airte Bwana Jackson Mmbando akiongea na wasanii chipukizi
wa Kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro wakati Airtel ilipotembelea
vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace
Mkoani humo.
Wasanii chipukizi kutoka morogoro watembelewa katika vijiwe vyao na kujiunga na mashindano ya Airtel Trace.
Kampuni
ya simu za mkoni ya Airtel imeendelea kuwafikishia wateja wake na
wapenzi wa muziki katika mikoa mbalimbali na kuwaunganisha katika
mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi ya Airtel Trace
yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel
imetembelea Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace
music star katika vijiwe mbalimbali mkoani hapo.
Akizungumza
na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali
mjini Morogoro, Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema
huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye kipaji cha kuimba kujiunga
na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba 0901002233 kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma.
Mashindano
haya yanatoa mwanya wa watanzania wenye ndoto za kuwa wanamuziki nyota
kupata fulsa ya kuzifikia ndoto zao. Sambamba na hilo tutakuwa na
washindi watakaojishindia zawadi mbalimbali hapa nchini kama vile pesa
taslimu na nafasi ya kushinda na kushiriki mashindano ya Afrika
yatakayofanyika nchini south Afrika na kushirikisha washindi wengine
toka nchi 13 barani afrika ambabo Mshindi wa Afrika atapata nafasi ya
nafasi kwenda kurekodi wimbo wake nchini Marekeni na kupata mafunzo ya
muziki kutoka kwa msanii nguli wa muziki Akon huko nchini Marekani
Nao
baadhi ya wasanii waliokutwa kwenye vijiwe vyao waliweza kushiriki
shindano hilo kwa kurekodi nyimbo zao kupitia Airtel Trace muziki star
huku wakiishukuru Airtel kwa kuwaletea huduma ambayo itawakomboa wasanii
chipukizi wasio na uwezo.
Ambapo
Hamis Ramadhan aka brash waya 2 alikuwa na haya ya kusema” tunashukuru
Airtel kwa kutuletea mshindano haya kitaani kwani tunavipaji lakini
tunashindwa kupiga hatua kwakuwa uchumi ni mdogo tunaamini kwa kuppitia
Airtel Trace tutatoka , kukubwa ni kusaidia na kupigiana kura ili
tufanikiwe, tunaamini Airtel Trace Tanzania Atatokea Morogoro na hivyo
natoa wito kwa wanamorogoro wajiunge kwa wingi na kutumia nafasi hii ili
kubuka kuwa masuper star.
Kwa
upande wake Ramadhani Nguyao alisema “ nimefurahia mpango mkubwa na
wakwanza Tanzania utakaowawezesha wasanii chipukizi kupata fulsa ya
kuimba na kurecord wasanii wakubwa kama Akon. Mimi nimevutia na
ntajiunga na mashindano haya na waomba watanzania wengi na wasanii
wenzangu wa Morogoro na nje ya Morogoro kujiunga na kushiriki katika
mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.
Mashindano
ya Airtel Trace Music Stars yalizinduliwa rasmi nchini Mwanzoni na
October na yatadumu kwa muda wa mienzi sita ambapo fainali ya mashindano
haya inategemea kufanya Mwaka kesho Machi 2015 nchini South Afrika.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment