Watu 24 wameuawa mjini Baidoa
Kusini mwa Somalia wakitizama mechi baina ya Manchester United na
Arsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na Al Shabab.
Taarifa
za awali zinaeleza kuwa milipuko miwili mikubwa ilitokea, katika mkahawa
huo uliokuwa umejaa mashabiki wa mechi kati ya Manchester United na
Arsenal.
Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo.
Mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji waislamu wa Al-Shabaab mwaka wa 2008, lakini walitimuliwa mwaka 2012.
Mji
huo ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu ni mji wa
hivi punde zaidi kushambuliwa na wanamgambo hao wa kiislamu.
Shambulizi
la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na
viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa
bomu.
Walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa muungano wa Afrika AMISOM.
Shambulizi hili limetokea muda mchache tu baada ya kukamilika kwa warsha ya viongozi wa mataifa yanayochangia wanajeshi wake katika jeshi la muungano wa Afrika AMISOM.
Siku ya ijumaa watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika mgahawa mwengine kufuatia shambulizi la Al Shabaab.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment