May 13, 2018

 
UTASHANGAA lakini ni ukweli na uhakika kuwa mtu mmoja anayeitwa Glenn Thompson ndio ameshika utamu wa dunia kwani kazi yake ni kupanga ratiba ya Ligi Kuu England.
Thompson, ambaye ni raia wa Uingereza ndio mpangaji wa furaha, mihemko na hasira za mashabiki wa soka duniani kote wanaofuatilia Ligi Kuu England.

Anaishika dunia kuanzia mwezi Agosti ya kila mwaka hadi mwezi Mei, ambapo mashabiki wa soka wanakuwa na mzuka mkali wa ligi ya England.

Thompson ni mtaalamu wa kompyuta katika Kampuni ya Atos, ambayo ndio yenye jukumu la kupanga ratiba na kukotoa msimamo wa ligi hiyo.

Atos, ambayo ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya teknolojia ya kompyuta yenye makao yake makuu mjini Bezons nchini Ufaransa imekuwa inafanya kazi hiyo tangu Ligi Kuu England ianzishwe mwaka 1992.
Thompson hutumia kompyuta maalum, ambayo imepewa jina la `The Fixture Computer’ (Kompyuta maalum ya ratiba), kwa ajili ya kupanga ratiba ya ligi zote za England. Kuanzia Ligi Kuu England hadi Ligi Daraja la Nne.
Kutokana na umaarufu wa Ligi Kuu England duniani kote ndiyo maana mara zote mashabiki wamekuwa wanasubiri kwa hamu ratiba.
Ligi Kuu England ya msimu wa 2018/19 inamalizika leo Jumapili katika viwanja mbalimbali wakati ambao bingwa alishapatikana.

Baada ya ligi kumalizika leo, watu wataanza kusubiri kwa hamu ratiba ya msimu wa 2018/19.
Ratiba ya Ligi Kuu England kwa msimu wa 2018/19 inatazamiwa kutolewa Juni 14, mwaka huu wakati ligi inatazamiwa kuanza Agosti 11, mwaka huu na kumalizika Mei 19, 2019.

Ligi Kuu England ndio inaongoza kwa kutazamwa viwanjani na kwenye televisheni duniani kote.
Utafiti unaonyeshwa kuwa watu wapatao bilioni 4.7 wanatazama ligi hiyo kupitia televisheni na mitandao ya kijamii.
Kutokana na watu wengi kuifuatilia ligi hiyo ndio maana unahitajika umakini mkubwa wakati wa kupanga ratiba.
Mashabiki wengi hufuatilia kuona timu zao zitaanza na timu gani na mechi dhidi ya wapinzani wao wa jadi zitachezwa lini.

Mashabiki hupenda kujua timu yenye ratiba rahisi au iliyopangiwa timu ngumu.

Kanuni za kuzingatia upangaji ratiba
Thompson anasema kuwa wakati wa upangaji ratiba kuna kanuni ambazo lazima zizingatiwe.
Kwa mfano katika kila mechi tano, kila timu lazima iwe na mechi mbili nyumbani na mechi tatu za ugenuni.
Thompson anasema kuwa suala jingine la kuzingatia ni kuhakikisha kuwa hakuna timu inacheza mechi zaidi ya mbili ugenini au nyumbani mfululizo.

Wakati wa upangaji huo, Thompson wakati akipanga ratiba lazima awasiliane na wadau wa ligi yaani Chama cha Soka England (FA) na klabu za soka zinazoshiriki Ligi Kuu England.
Ili kupanga ratiba hiyo kwa ufanisi, Thompson hutumia utaalamu wake na tekinolojia ya kiwango cha juu ya kompyuta.

Thompson kila msimu ana jukumu la kupanga ratiba ya mechi 2,036 za msimu wa ligi ya England.
Tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya England mwaka 1992, Glenn amepanga ratiba ya karibu mechi 60,000.
Gazeti la Daily Telegraph la Uingereza liliwahi kumtaja Thompson kama miongoni mwa watu wenye nguvu zaidi England.
Pia jarida la ‘Four Four Two’ limemtaja kama miongoni mwa watu 100 wenye nguvu katika medani ya soka duniani.

Namna ya ratiba inavyopangwa
Thompson anaelekeza kuwa timu 20 za Ligi Kuu England hugawanywa katika makundi matano.
Makundi hayo huwa na timu nne ambazo zinapangiwa mechi za nyumbani na ugenini.
“Wakati wa hupanga timu hizi katika seti huwa tunahakikisha timu za sehemu moja zinatenganishwa,” anasema Thompson.
Mfano timu zinazotoka eneo moja za Manchester City na Manchester United au Liverpool na Everton huwa hazipangiwi kucheza katika eneo lao kwa wakati mmoja wakati wa wikiendi ya mechi za Ligi Kuu.
Pia klabu huwa zina uhuru wa kuomba baadhi ya siku wasipangiwe mechi kwenye viwanja vyao nyumbani kutokana na sababu za kiusalama.
Thompson anaeleza mara baada ya kukamilisha kupata ratiba ya awali huhakikisha anawasiliana na Kamati ya Ligi na Chama cha Soka England kwa ajili ya uhakiki.
Kwani kwa mfano kuna uhakiki inabidi ufanywe ili kupachika ratiba ya mechi za Kombe la Ligi, Kombe la FA, mashindano ya Ulaya na mechi za kimataifa.
Thompson anasema pia wana utaratibu maalum wa kupanga ratiba ya mechi zinazochezwa kipindi cha sikukuu ya krismasi na mwaka mpya.
“Timu ikicheza sikukuu ya Boxing Day kwenye uwanja wa nyumbani basi lazima wakati wa mwaka mpya icheze ugenini au kinyume chake,” anafafanua Thompson.

Kuepusha malalamiko
Thompson anaeleza pia kila mwezi Machi, Kamati ya Ligi Kuu England hutoa fomu kwa ajili ya timu kujaza.
Fomu hizo huwa na mambo matatu nayo, ambapo timu huulizwa kama kuna siku maalum wanapenda wawe na mechi ya nyumbani na majibu ya swali hili hutakiwa kuambatanishwa na mapendekezo ya polisi.
Pia timu hupewa nafasi ya kuchagua klabu wanayopenda kukabiliana nayo siku hiyo.
Katika kipindi cha sikukuu ya Boxing Day, pia timu hupewa nafasi ya kuchagua timu ambayo watapenda kukabiliana nayo siku hiyo.

Related Posts:

  • Watoa huduma wa afya wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepukan na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ili kuhakikisha takwimu za vifo vya akina mama wajawazito haziongezeki kama ilivyo sasa  kwani… Read More
  • Eid EL Fitri: Waislam watakiwa kuitunza Amani   Waislamu duniani kote leo hii wameswali swala ya Eid ul-Fitr 2018. Mkoani Morogoro licha ya misikiti Mingio kuendesha Ibada hiyo. lakini sisi tunakuletea Ibada iliyoswaliwa kati viwanja vya The Islamic Foundition j… Read More
  • Miss Morogoro 2018, yazinduliwa Rasmi Samaki Spot Mratibu Mkuu New Miss Morogoro 2018 Farida Kilususu akizungumza na ummati wa wahudhuliaji usiku wa jana pale Samaki Spot Pazia, lishafunguliwa rasmi, mwenye macho na haone, wamasikio wasikie. Ndiyo kauli tunayoweza kui… Read More
  • Eid al Fitr : Makkah Eid al Fitr 1439 Khutbah Sheikh Humaid   Kutokea Makkah, tunakuletea Khutbah ya  Eid al Fitr  kama ilivyoongozwa na Sheikh Humaid                   &n… Read More
  • Official Video: Sihitaji - Strevol Kutoka mji kasoro Bahari Morogoro, maeneo ya Forest ndani ya studio za Kwanza Record chini ya mtayarishaji Vennt Skillz, Mokomoko Movemennt inamdondosha kwenu na kumtambulisha rasmi zao lingine kabisa chini ya Lebo hiy… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE