Habari hizi zikufikie wewe mkazi wa mji wa Morogoro. Almashauri ya Manispaa ya Morogoro na kampuni ya ujenzi wa soko kuu la mkoa , wametupatia picha rasmi za muonekano wa soko kuu la mkoa wa Morogoro likiwa katika muonekano wa mwisho yaani jinsi litakavyokuwa. Kwa sasa ujenzi unaendelea katika eneo lilipokuwa soko la awali ambalo lilijengwa mwaka 1953. Kwa mujibu wa mkandarasi toka kampuni ya Ujenzi ya NCC, ametuambia kwamba soko hilo linatarajiwa kukamilika mwezi wa nane mwaka 2019.
November 27, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment