Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga ameyanusuru maisha ya kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwita Marwa mkazi wa Kemakorere baada ya kudaiwa kufanyiwa tohara isiyo Salama.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa msaada huo baada ya kumkuta kijana huyo akiwa ameanguka barabarani bila ya kupatiwa msaada wowote na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.
Mkuu huyo wa wilaya alikuwa njiani kuelekea Nyamongo katika ziara yake ya kikazi.
Inadaiwa kuwa kijana huyo alifanyiwa tohara hiyo isiyo salama huko porini na kuvuja damu nyingi zilizopelekea kuishiwa nguvu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment