Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete (kushoto) akipokea Katiba Inayopendekezwa toka kwa aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wa
sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo iliyofanyika jana 8 Oktoba, 2014
mjini Dodoma.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed
Shein (kushoto) akikabidhiwa Katiba Inayopendekezwa toka kwa aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wa
sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo iliyofanyika jana 08 Oktoba, 2014
mjini Dodoma.
Marais
wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakikata
utepe kufungua Katiba Inayopendekezwa wakati wa sherehe ya makabidhiano
ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Marais
wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakionyesha
juu Katiba Inayopendekezwa ili wananchi waweze kuziona wakati wa sherehe
ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DODOMA).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakiwa
wameinua…
KATIBA INAYOPENDEKEZWA YAKABIDHIWA RASMI KWA WAHESHIMIWA MARAIS WA
TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
09/10/2014.
KATIBA
Inayopendekezwa imekabidhiwa rasmi 8 Oktoba, 2014 kwa Waheshimiwa Marais wa
Tanzania Bara, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja Rais wa Zanzibar, Mhe.
Ali Mohammed Shein.
Akihutubia
wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kuwa tukio hilo la
kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa ni jambo la kihistoria kwa nchi ya Tanzania
na linaashiria kukamilika rasmi kwa kazi ya lililokuwa Bunge Maalum la Katiba
lililoanza tarehe 18 Februari mwaka huu.
Mhe.
Dkt. Kikwete alisema kuwa ni hatua nyingine ya kihistoria ya nchi kwani hatua
ambayo imesalia hivi sasa ni ile ya wananchi kwenda kuipigia kura za maoni
Katiba hiyo ili waweze kufanya uamuzi kuhusiana na Katiba hiyo na endapo
wananchi hao wataikubali basi Tanzania itakuwa imejipatia Katiba mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Sina
budi Kumshurkuru Mwenyezi Mungu kwa hapa tulipofikia na sina budi kumshukuru
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel John Sitta, Makamu wake Mama
Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya, nawashukuru pia
Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum kwa uongozi waa makini, natoa
pia shukurani za pekee kwa Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa
kukamilisha kazi hii tena mmeikamilisha kazi hii kwa kiwango cha juu sana cha ubora”,
alisema Mhe. Dkt. Kikwete.
“Shukurani
zangu pia ziende kwa Katibu wa Bunge Maalum na Naibu Katibu pamoja na Wasaidizi
wao wote kwa kazi nzuri walioifanya na kuiwezesha Bunge Maalum la Katiba
kukamilisha kazi yake kwani haikuwa kazi rahisi hata kidogo”, aliongeza Mhe.
Dkt. Kikwete.
Naye
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein
alimpongeza Rais wa Tanzania Bara, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kuanzisha mchakato huo wa kupata Katiba mpya na alitoa pongezi zake kwa
Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samule Sitta pamoja na
Makamu wake Mhe. Samia Suluhu ikiwemo pongezi pia kwa Wajumbe wote walioshiriki
katika mchakato huo.
Katika
Hotuba yake, Mhe. Dkt. Shein alisema kuwa katika mchakato mzima wa kutafuta
Katiba hiyo, Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu kwani hakuna hata hatua moja
ambayo haikushiriki.
“Nataka
leo nisisitize kuwa Zanzibar ibaki sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika kila hatua ya mchakato huu imeshirikishwa na kushiriki kikamilifu hadi
hivi leo tulipofikia”, alisema Dkt. Shein.
Naye
aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa lililokuwa Bunge Maalum la
Katiba. Mhe. Andrew Chenge alisema kuwa ndani ya Katiba hiyo katika eneo la
Uongozi, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania imeweka Ukomo wa idadi
ya Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri ambapo kwa mapendekezo hayo, idadi ya
Mawaziri na Naibu Mawaziri haitazidi 40.
Mhe.
Chenge alifafanua kuwa idadi hiyo ya Mawaziri na Naibu Mawaziri itaisadia
Serikali na Wananchi kupunguza gharama kwa ujumla na pia katika suala hilo hilo
la uongozi aliongeza kuwa Rais wa Zanzibar anapokuwa Makamu wa Rais ni ishara
ya Muungano, hivyo itaisadia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kudumisha Muungano
uliopo.
Aidha,
Katika masuala yanayohusu Bunge, Chenge ameeleza kuwa Katiba inayopendekezwa
inapendekeza mambo mawili ya msingi ambayo ni Uwiano wa Wabunge pamoja na Ukomo
wa Idadi yao.“Kuhusu
Uwiano wa Wabunge, inapendekezwa kuwepo na uwiano ulio sawa kati ya Wabunge
Wanaume na Wabunge Wanawake uwe asilimia hamsini kwa hamsini”, alisema Chenge.
Akiongea
kuhusu suala la ukomo wa Wabunge hao, wote wa kuchaguliwa na wale wa kuteuliwa,
Mhe. Chenge alibainisha kuwa idadi hiyo haitapungua 340 na haitazidi 390.“Mhe.
Rais, Katiba hii Inayopendekezwa imesheheni malengo muhimu, ya Kiuchumi, ya
Kisiasa, kijamii, ya kiutamaduni na kimazingira”, alisema Chenge.
Aliongeza
kuwa katika malengo ya Taifa na kijamii yameboreshwa zaidi kwa kuweka mazingira
yatakayowezesha Wasanii pamoja na Wanamichezo kukuza na kuendeleza vipaji vyao
na kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment