
MWAMBUSI ameiambia mkazuzu.com amechukua uamuzi huo akiwa na lengo la kupumzika kwa msimu mmoja kama wanavyofanya makocha wengine duniani akimtolewa mfano kocha wa sasa wa MANCHESTER CITY PEP GUARDIOLA alivyoamua kupumzika alivyoachana na BARCELONA.
Kocha huyo ambaye kwa siku mbili hizi yupo mkoani MOROGORO kwa shughuli zake amesema baada ya mapumziko yake ndipo atakapoamua kwenda wapi.
JUMA MWAMBUSI alijiunga YANGA kama kocha msaidizi miaka miwili iliyopita akitoka MBEYA CITY ambapo alikua kocha mkuu.
Akiwa na YANGA amefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili, kombe la FA mara moja na kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi kombe la shirikisho barani AFRIKA msimu wa mwaka 2016.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment