November 28, 2015

 
Alfonce Mawazo enzi za Uhai wake
Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), leo wamewaongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Mwanza kutoa heshima za mwisho, za kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo.

 

Katika shughuli hiyo baba mdogo wa Marehemu Alphonce Mawazo, Charles Lugiko na mtoto mkubwa wa Marehemu Prescious Mawazo wakatoa ujumbe mzito, huku mwanaye anayesoma darasa la nne akiahidi kuwa siku moja atarithi mikoba ya baba yake katika ulingo wa Siasa.

 

 
Aliyekuwa Mgombea Urais wa CHADEMA na kupeperusha bendera ya UKAWA, Mhe. Edward Lowassa akitoa salamu zake za mwisho kwa aliyekuwa M/kiti CHADEMA moa wa Geita Alphonce Mawazo aliyeuwawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga 

Safari ya kuusindikiza Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, imeanzia hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza, ambapo mwili wake ulihifadhiwa kwa kipindi cha siku takribani kumi na nne, tangu mahuti hayo yalipomkuta Novemba 14 mwaka huu.

 

Kituo cha kwanza cha safari hii kikawa nyumbani kwa baba yake mdogo kata ya Luchelele Nyegezi eneo la Sweya, ambapo taratibu mbalimbali za kifamilia zimefanyika, kabla ya kuanza safari ya kuupeleka mwili wake katika viwanja vya Furahisha kwa ajili ya kuagwa.

 

 

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akitoa salamu za mwisho kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita kamanda Alphonce Mawazo ambaye ameagwa kitaifa katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza
 

Taratibu hizo zilipokamilika safari ya kuelekea katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza ikawadia, ambapo katika viwanja hivyo viongozi wa Kitaifa wa (Chadema) wakaungana na mamia ya wakazi wa mkoa wa Mwanza kutoa heshima za mwisho.
 
Baada ya shughuli hiyo wafuasi wa Chama hicho wakaungana katika safari ya kuusindikiza mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, hadi mkoani Geita ambako utahifadhiwa katika Hospitali ya wilaya hiyo, kwa ajili ya kuagwa siku ya Jumapili katika viwanja vya Magereza.
 
Shughuli hiyo itakapokamilika Mwili wake utapelekwa katika mji mdogo wa katoro, ambako aligombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuagwa, kabla ya safari ya kuelekea Kijijini kwao kata ya Chikobe, ambako mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu majira ya saa nne asubuhi.
  
 Familia ya Marehemu Alphonce Mawazo wakiendeshwa na mchungaji kwa ibaa fupi iliyofanyika nyumbani kwa baba Mdogo wa Marehemu.
  
Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo ikiwasili nyumbani kwa baba mdogo (Charles Lugiko) Nyegezi jijini Mwanza ukitokea Hospital ya Bungando kwaajili ya ibada fupi
  

 
  Kwa mara nyingine tena mwanamuziki anayefanya poa katika anga la bongo fleva Chibau mtoto wa Pwani , anakuja tena na ngoma yake mpya kabisa inayoitwa Mademu. Katika wimbo huu Chibau amemshirikisha Nay True Boy ambaye naye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Nyumbani kwetu pamoja na Suprano.
 Wimbo umefanyika katika studio za Free Nation chini ya mtayarishaji machachari nchini Mr: T
 
 Live and Die in Afrika is the "LIVE AND DIE IN AFRIKA" album title track . The album is a celebration of the African continent coming of age, flaunting the richness in cultural diversity , talent and resources. And now we finally have a generation that fully believes in this continent and her great potential.African diaspora is on a mission to reconnect with their roots, be it through music or other media. There is a willingness to aspire everything and anything African. “In California, they have been dancing to Sura Yako,” (Barack Obama). They sing and dance to the same tune at a wedding in Moshi, Tanzania. There is a willingness to Live and Die in Afrika. These are the united minds of Africa. Minds that will LIVE AND DIE IN AFRIKA!

Live and Die in Afrika Music video was shot in Nairobi, Kenya.
Audio produced under Sauti Sol Entertainment.
Styling by Annabel Onyango.
          

  majaliwa 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, amewasimamisha kazi watumishi wengine watatu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili.
Watumishi hao hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 




http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/11/image-28-11-15-14_58.jpeg
Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanuzi wa maagizo ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo yalazima katika Wizara, idara na taasisi za serikali.
Katika ufafanuzi huo Balozi Sefue amemtaka kila mtendaji mkuu ama Afisa Masuhuli wa Serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

November 27, 2015


Watu kumi na nane wameuawa na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea shambulio la kigaidi Kusini-Mashariki mwa Niger, karibu na mpaka na Nigeria.

Shambulio hilo linahusishwa wanajihadi wa kundi la Islamic State, kundi la kiislamu la Afrika Magharibi, linalojulikana kama Boko Haram.

Aidha inaelezwa kuwa zaidi ya nyumba mia moja zimechomwa moto na huku wana  ikidaiwa kuwa watoto wawili wameteketea moto katika tukioh ilo baya

Inaelezwa kuwa baada ya wapiganaji hao kufanya mauaji katika kijiji cha Gogone waliondoka kwa mguu, kuelekea kijiji jirani kilomita kumi na tano kutoka mji wa Bosso, karibia na mpka wa Niger na Nigeria.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Uganda kwenye sehemu ya pili ya ziara yake Afrika.
Papa amelakiwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Baadaye, Papa anatarajiwa kuelekea ikulu ya Rais mjini Entebbe, kisha ahutubie maafisa wa serikali na mabalozi humo ikuluni.
Baadaye atawahutubia walimu.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pia yumo nchini Uganda kukutana na Papa Francis.
Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga anasema Vatican imevutiwa na ukosefu wa usalama pamoja na uhusiano kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Wawili hao watakutana katika ikulu ya rais wa Uganda mjini Entebbe.
Papa Francis atakuwa Uganda hadi asubuhi ya Novemba 
Bofya hapakupata ratiba nima ya ziara ya papa
Singer Name:- Chief Maker
  

Song Name:- Viro Sakata
  

Country;- Tanzania
 

 Genre;- Bongo Flavour
  

Director:- Abdul Omary
           
Mwanaa FA, 201444444444444 
 Mkali wa kuandiki mziki wa Hip Hop Tanzania Hamis Mwinjuma Mwana FA, aemtoa Cover ya wimbo wake mpya unaoitwa "Ahsanteni kwa kuja"
  Wimbo huwo mpya wa FA,  umetayarishwa chini ya producer Hermy B & Pancho Latino kutoka B Hitz Music Group.
Wewe i shabiki wa FA kama mimi na Saddiq Kisimikwe? kaa mkao wa kula

November 25, 2015



1cst
 Leo Chama cha Haki Miliki Tanzania ‘COSOTA’ wameendesha Semina ya Ufuatiliaji wa kazi za sanaa na Ugawaji Mirabaha ambayo itakusanywa na vituo vya Radio na Televisheni.
Hii itakua ni fursa ya Wasanii mbalimbali wa Tanzania kulipwa na vituo vya Radio na Tv kila ambapo nyimbo zao zitakapokuwa zinapigwa ambapo waliohudhuria katika semina hiyo wasanii, Watayarishaji wa muziki na Mameneja.
Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na Babu Tale, Mchizi Mox, Meneja Maneno, Mona Gangstar, Nikk wa pili, Nikki Mbishi, Jaymoe, Lamar na wengine wengi.
2cst

4cst

5cst

7cst
Nassib Abdul Juma au Diamond Platnumz ameshika namba moja kwenye orodha ya Wasanii bora 15 wa Afrika mwaka 2015 ‘Top 15 African Artist of 2015’ ya Tuzo za African Music Magazine Awards [AFRIMMA.]
1plat
Waandaji wa tuzo hizo wametoa orodha hiyo kupitia website yao ambapo Diamond Platnumz ameshika namba moja akifuatiwa na Wizkid kwenye nafasi ya pili, Olamide kwenye nafasi ya tatu na na Davido akiwa kwenye nafasi ya nne.
Hivi ndivyo walivyoandika kwenye website yao
Number 1 Diamond Platnumz Your guess is as good as ours, Diamond Platnumz the golden boy of East Africa and Tanzania’s own music crown prince tops our list of Top 15 African Artists of 2015, Flamboyant, exciting and creative Diamond Platnumz has emerged as the new face of East African music and the undisputed King of Bongo flava. Never before has an artiste dominated the Tanzanian musical landscape like Diamond is presently doing lifting the East African flag to lofty heights on the world stage. Seen as a spoilt child by his siblings with the way his mother took him around to tale to shows every time and wait for him till late in the night for him to perform, Diamond has gone on to justify the unshaken faith of his mother in his musical ability emerging as one of Africa’s brightest music stars.
Born on October 2nd, 1989 as Nasibu Abdul Juma in Dar REs Salam, Diamond Platnumz started his music career as a rapper dreaming of becoming a rap star and getting all the girls but he found fame as a singer with his special brand of bongo lava. The very prolific artist has recorded more than 140 songs in his music career and is seen as the poster boy of Tanzanian/East African music. The song ‘Number One’ and the subsequent remix featuring the flaming Davido has catapulted Diamond to the top of the African music game with his popularity soaring more than ever before. The energetic performer has shut down venues all over Africa and beyond with fans yearning for more.
Diamond is a music person who listens to music all the time and is absolutely loved and adored by his fans while setting an unprecedented record of winning 7 Tanzanian Music Awards in one go. The BET Awards 2014 nominee stormed AFRIMMA with multiple nominations and he won in the Best Male East Africa category before going on stage to rekindle his partnership with Davido on the ‘Number One’ remix. 2015 has seen Diamond Platnumz cement his status as Africa’s number one artist with multiple awards including MTV EMA’s and AFRIMMA 2015 Artist of The Year Award.”
Kwenye tuzo za Afrimma mwaka huu zilizofanyika Oct. 10 Dallas, Marekani, Diamond alishinda tuzo 3, ikiwemo ya Msanii Bora Wa Mwaka

November 24, 2015


BEN 1
.Wanamuziki Ben Paul na Fid Q wanaoshiriki kwenye  onyesho la Coke Studio wakiwa katika picha ya pamoja na washabiki wao wakati wa uzinduzi wa onyesho hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
BEN 2
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Coca Cola Kwanza wakifuatilia onyesho la Coke Studio.
BEN 3
Msimu wa Coke Studio umewahusisha pia wanafunzi mashuleni kuonyesha vipaji vyao kama anavyoonekana mwanafunzi akionyesha kipaji cha kucheza katika moja ya tamasha la Coke Studio lililofanyika mjini Mwanza hivi karibuni.
Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva nchini Ben Paul amesema kuwa ushiriki wake katika onyesho la Coke Studio ni moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki.
Katika mahojiano aliyoyafanya wiki hii kuhusiana na ushiriki wake katika onyesho hili maarufu linaloendeshwa na kampuni ya Coca-Cola na kushirikisha kolabo za wanamuziki mbalimbali wa Tanzania na nje ya nchi alisema anajivunia ushiriki wake katika onyesho hili na ameweza kujifunza mengi kuhusiana na fani ya muziki.
“Japo hapo awali nimewahi kushinda tuzo mbalimbali za muziki lakini ushiriki wangu katika onyesho hili  kubwa la kimataifa ni moja ya mafanikio yangu makubwa katika safari yangu ya muziki.
Alisema anajisikia fahari  kufanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki Wangechi kutoka nchini Kenya katika msimu huu wa Coke Studio ambapo kwa hapa nchini onyesho hilo linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia luninga ya Clouds.
Ben Paul alisema onyesho la Coke Studio linahamasisha vijana kujiamini na kuonyesha vipaji vyao na aliwataka vijana wenzake kujiamini na kutokata tamaa iwapo wanataka kutimiza ndoto zao na kufanikiwa katika maisha.
Alisema katika safari yake ya muziki amekutana na changamoto nyingi mojawapo ikiwa ni kunyimwa nafasi ya kurekodi nyimbo zake na waandaaji mbalimbali wakiamini kuwa hakuwa na uwezo wa kuimba lakini licha ya kufanyiwa hivyo aliendelea kupambana mpaka kufanikiwa kufika alipo sasa.
“Ninachotaka kuwaambia ni kwamba, mfano, kwa wale wenye vipaji vya kuimba, kitu kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa na nyimbo nyingi ambazo, hata ukirekodi moja isipofanya vizuri, unatoa nyingine ili kuhakikisha unaendelea kusikika masikioni kwa watu”, alisema
Aliwaasa vijana wa jinsia zote  kujiamini na kuondokana na dhana kwamba jinsia fulani ndio wanaweza  kufanya kitu fulani na kusisitiza kuwa kila mtu ana kipaji na anaweza kufanya mambo makubwa.
Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao wako nao katika msimu huu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu. Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up) na Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face kutoka Nigeria na Ali Kiba ambaye amefanya Kolabo  na mwanamuziki Victoria Kimani.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga  kushirikiana na wasanii wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao
Onyesho la Coke Studio linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia luninga ya Clouds. Pia unaweza kusikiliza kipindi cha Coke Studio kwenye Clouds FM kila Jumamosi saa nne asubuhi.
Kesi imeendelea Mahakama Kuu Mwanza leo November 24 2015, bado ni mwendelezo wa ishu ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita, Alphonce Mawazo… CHADEMA ilipata agizo kutoka kwa Mkuu wa Polisi Mwanza kuhusu kuzuiwa kuaga mwili wa kiongozi wao huyo aliyeuawa.
index
Ishu ikaenda Mahakamani jana na leo nina mengine kutoka Mahakama Kuu Mwanza >>> “Leo asubuhi tumepata ruhusa ya Jaji wa Mahakama kufungua kesi ya kudai haki ya kuzikwa marehemu Mawazo Mwanza.. tumefungua kesi mchana ambapo tumepeleka maombi matatu, kwanza tupate amri ya Mahakama inayotengua zuio la Mkuu wa Polisi Mwanza la kuzuia shughuli za uagaji wa mwili wa Mawazo isifanyike hapa Mwanza.”- John Mallya, Wakili wa CHADEMA.
                       index III
John Mallya akiongea na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Mwanza.

Maneno mengine ya John Mallya haya hapa nje ya Mahakama >>> “Ombi la pili ni kuiomba Mahakama itamke kwamba zuio hilo ni batili na kinyume cha sheria… Ombi la tatu ni kuomba Mahakama ikataze Mkuu wa Polisi Mwanza kujishughulisha na jambo lolote kuhusu mazishi na kuaga mwili wa Mawazo.”
index
Kesi imefunguliwa kwa hati ya dharura sana na itaendelea kesho saa tatu kwenye eneo la wazi, wananchi watapata fursa ya kusikiliza kesi hiyo.”- John Mallya.

Sauti ya John Mallya hii hapa, kutoka nje ya Mahakama Kuu Mwanza leo.


na picha ni kutoka Millardayo.com
Tokeo la picha la nyumbani kwetu - nay
Mkali wa muziki wa Rap nchini Tanzania anyefanya poa sana mpaka nje ya Tanzania kwa sasa Nay wamitego, baada ya kufanya poa na audio ya wimbo wake wa Nyumbani kwtu, wimbo ulioimbwa katika mahadhi ya mnanda, sasa ametuletea video ya wimbo huwo. Nay ambaye nyimbo zke nyingi zimekuwa hit, anaamini kabisa video ya wimbo wa nyumbani kwetu utakufanya uzidi kufurahi kazi zake anamaliza kwa kusema 

            
Mwanamuziki mkali wa sauti Tanzania Rich Mavoko leo hii ametuletea ngoma yake mpya kabisa inayoitwa, Naimani. Kumbuka kwamba Rich Mavoko kwa mara ya September 2014 ndiyo aliachia wimbo wake   mwisho unaofanya poa mpaka leo wimbo wa pacha wangu 

Sikiliza na Download hapa
   

November 23, 2015



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Kwa mujibu wa  Sheria ya Sikukuu za Kitaifa  (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike  kwa kufanya kazi.  Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu  (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu.  Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi,  fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.

Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo,   sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015

November 22, 2015

0a71d082-9c10-4605-923a-0e0777004614
Pichani ni watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15  mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya misheni Rulenge. Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.
Baada ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni. Msamaria  amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa.
Inaelezwa na ma daktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.
Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchaango kwake ili aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.
Baba Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana uwezo hata wa kufika Dar es Salaam.  Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.

  

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Africa, mtanzania Nalimi Mayunga aliwasili nchini Marekani toka November 17 2015 kwa ajili ya kufanya kolabo na mwimbaji Akon, video ikimuonyesha akiwa na Akon nyumbani kwake huko Los Angeles ndio hii hapa chini

               

November 22 michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA iliendelea kwa michezo miwili kupigwa, timu ya taifa ya Tanzania bara ambapo inafahamika kama Kilimanjaro Stars ilishuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Somalia.
Taifa Stars forward John Bocco (right) is guarded by a South Africa's Under-23 team defender during a friendly match at Eldorado ground. Stars lost 2-0. Kili Stars will be formed by majority of the national team squad. photo | courtesy of salehjembe blog
Stars ambao wapo chini ya kocha King Kibadeni walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-0, magoli ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na nahodha wao John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 12, Elias Maguli dakika ya 17 na 54 na dakika moja baadae John Bocco akapachika tena goli la nne.

IMGS2612

IMGS2612
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipomtembelea nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma Novemba 21, 2015.
IMGS2602
  Mke wa Waziri  Mkuu, Mama Mary Majaliwa  (kushoto) akikaribishwa na mke wa Waziri Mkuu, Mstaafu Mama Tunu Pinda wakati alipowasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda katika kijiji cha  Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa mazungumzo Novemba 21, 2015 
IMGS2627
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu,Mstaafu Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia) Wakati Waziri Mkuu alipomtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma Novemba 22, 2015. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar
Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake.
Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia.
Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa.
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma" nini maoni yako kuhusiana na taarifa hii kutoka kwa kiongozi wa chama cha ACT Zitto Kabwe?????

November 21, 2015

Wagombea watano wa tuzo ya BBC kwa mwanasoka bora wa mwaka 2015 wametangazwa kwenye hafla maalum iliyoandaliwa mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mshindi wa tuzo la mwaka 2014 Yacine Brahimi, yupo kwenye orodha hiyo pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang, André Ayew, kutoka Ghana, Sadio Mané na Yaya wote wa Ivory Coast.
Mshindi ataamuliwa na mashabiki wa soka Afrika ambao watapewa fursa kupiga kura hadi tarehe 30, Novemba.
Unaweza kupiga kura mtandaoni kwa kubofya hapa au kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa nambari +44 7786 20 20 08:
  • Ujumbe 1 kwa-Emerick Aubameyang
  • Ujumbe 2 kwa André Ayew
  • Ujumbe 3 kwa Yacine Brahimi
  • Ujumbe 4 kwa Sadio Mané
  • Ujumbe 5 kwa Yaya Touré
Gharama za matumizi ya simu za kimataifa itatumika, tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako. Ujumbe moja utatumika kwa nambari moja ya simu pekee.
Mshindi atatangazwa ijumaa tarehe 11 mwezi December wakati wa matangazo maalum kwenye BBC World News na BBC World Service, wakati mitandao ya BBC Sport na BBC Africa ikitoa pia matangazo. Kwa sheria na masharti bofya hapa.
Wagombea wa tatu mwaka huu waliopigiwa kura na wanahabari 46 kutoka Afrika wamewahi kushinda tuzo hilo: Ayew (2011), Touré (2013) na Brahimi (2014).
Aubameyang ameorodheshwa kwa mwaka wa tatu mfululizo wakati Mané akijumuishwa kwa mara ya kwanza.
Mshambulizi Aubameyang amenawiri katika ufungaji magoli mwaka huu, akimaliza kama mfungaji mabao bora wa Borussia Dortmund msimu uliopita kabla ya kuandikisha rekodi mpya ujerumani kati ya 2015-16.
Mwezi Oktoba raia huyo wa Gabon, mwenye umri wa miaka 26,alikuwa mtu wa kwanza kufunga bao katika mechi nane za mwanzo katika Bundesliga huku mechi zake 17 za mashindani zikiishia ushindi mkubwa wa mabao 20 .
Mwaka huu pia umeshuhudia mafanikio makubwa kwa Ayew na ingawa haikuwa kilele, kombe la mataifa barani Afrika yalipunguza machozi yake huku the Black Stars ikishindwa na Ivory Coast.
Alikuwa na ushawishi mkubwa katika kampeni ya Ghana na kisha kuuhamisha ufanisi wake katika ligi guu ambako alifunga mabao matano katika mechi kumi alizochezea Swansea City.
Brahimi anayeichezea FC Porto amekuwa mchezaji anayelengwa barani Afrika na ulaya lakini raia huyo wa Algeria, 25, amekuwa akiongeza mabao katika ufanisi wake kwa kufunga jumla ya magoli 13 msimu uliopita huku akiisaidia klabu yake kushiriki robo fainali za ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita
Mojawepo wa mafanikio yake makubwa yalikuwa katika shindano hilo msimu uliopita ambako chenga chenga zake zingefananishwa tu na Eden Hazard wa Chelsea au nyota wa Barcelona Lionel Messi.
Tarehe 16 Mei, Mane anayeichezea Southampton alihitaji tu sekunde 176 kufunga hattrick ya haraka zaidi katika hisoria yake ya kucheza katika Premier League.
Ni miongoni mwa mabao yake 10 katika mechi 29 za Ligi ya Premia mwaka huu, matokeo yaliyoimarishwa zaidi hasa ikizingatiwa yeye ni mchezaji wa kiungo cha kati.
Mchezaji wa pekee katika orodha hii aliyewahi kunyakuwa kombe ni Touré na ilikuwa zawadi kubwa iliyoje wakati alipoiongoza Ivory Coast kunyakuwa taji la kwanza katika michuano ya kombe la mataifa katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.
Akiwa ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwaliko wapinzani wake, mchezaji huyo wa kiungo cha kati ni mhimili katika matumaini ya klabu ya Manchester City kunyakuwa mataji na kazi yake imetambuliwa na Fifa ambayo imemteuwa kama mchezaji wa pekee kutoka Afrika kuania taji la kifahari la Ballon d’Or.

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE